
SENEGAL: NYOTA wa Everton na Senegal, Idrissa Gueye amesema walishinda Kombe la Mataifa ya Afrika uwanjani na bingwa hawezi kuamuliwa ofisini.
Aidha, alisema yuko tayari kurejesha medali ya ubingwa kwa Morocco ikiwa hatua hiyo itasaidia kupunguza mvutano kati ya mataifa hayo mawili.Akizungumza baada ya mechi ya klabu yake ya Everton kushinda 3-0 dhidi ya Chelsea, Gueye alisema: “Niko tayari kukusanya medali na labda kuzirejesha kwa Morocco ikiwa hilo litapunguza mvutano kati ya nchi hizi mbili.”
Aliongeza: “Inasikitisha sana. Mechi ya mpira inashindwa uwanjani, na ndivyo tulivyofanya Morocco. Kwa mtazamo wetu, sisi ndio mabingwa wa Afrika. Mataji yanashindaniwa uwanjani, siyo maofisini.”
Licha ya msimamo wake huo, Gueye alieleza kutokubaliana na uamuzi wa shirikisho lao kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa CAF katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).




