Filamu

Genevieve Nnaji awa kivutio mkutano wa uwekezaji Nassau Bhamas

Nassau, BAHAMAS: MUIGIZAJI wa Nollywood Genevieve Nnaji amekuwa kivutio kikubwa katika Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa AfriCaribbean wa 2024 ambao ni Mikutano ya Mwaka wa Afreximbank uliofanyika huko Nassau, Bahamas.

Katika mkutano huo Genevieve aliongeza chachu ya kuwa kivutio kwake aliposimulia sababu yake iliyomfanya akatae fursa za kujiunga na kiwanda cha uandaaji wa filamu huko Hollywood Los Angeles nchini Marekani.

Mwigizaji huyo mzaliwa wa Jimbo la Imo mwenye umri wa miaka 45 alisimulia hayo hayo wakati alipokuwa mbele ya umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wa mwaka ambapo wengi walionekana kuvutiwa nak la alichokizungumza muigizaji huyo.

Nnaji alikuwa mmoja wa jopo la wanamkutano huo wa Biashara na Uwekezaji wa AfriCaribbean wa 2024 Mkutano uliangazia faida za miradi ya ubunifu kwa bara la Afrika, ambayo inasaidia biashara na uwekezaji katika sekta ya ubunifu, ikiwa ni pamoja na msaada wa kifedha.

Nnaji amesema awali hakufahamu kuwa alikuwa bidhaa muhimu na inayohitajika katika kiwanda cha filamu huko Hollywood lakini baadae aligundua kuwa yeye ni bidhaa inayohitaji wakati naye alihitaji nkujifunza zaidi ili awe lulu akiwa katika kiwanda hicho cha filamu cha Marekani.

Mwigizaji huyo alisema licha ya mafanikio ya filamu yake ya mwaka 2018 ya Lionheart, aliyopo Netflix, alihitaji msaada zaidi kutoka Hollywood ili afanye zaidi lakini kwa wakati huo alikosa.

Related Articles

Back to top button