Ligi KuuNyumbani

Geita yagoma kuswekwa mahabusu

KLABU ya Geita Gold imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Polisi Tanzania katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mabao ya Geita yamefungwa na George Mpole dakika 45 na Edmund John dakika 82 wakati bao la Polisi limefungwa na Hassan Kapona dakika 66.

Geita ilipoteza mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji kwa bao 1-0 Septemba 29 katika uwanja wa Liti mjini Singida.

Wakati huo huo Klabu ya IHefu imeambulia pointi ya kwanza katika ligi kuu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons katika uwanja wa Highland Estates, Mbarali mkoani Mbeya.

Bao la Ihefu limefungwa na Jaffary Kibaya dakika 55 wakati bao la kusawazisha la Prisons limefungwa na Ismail Mgunda katika dakika ya 86.

IHefu imepoteza michezo yote 4 ya awali ya ligi.

Related Articles

Back to top button