Habari Mpya

Geita Gold yapania kupindua meza

NAHODHA wa timu ya Geita Gold, Danny Lyanga amesema timu hiyo ipo tayari kupindua meza kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Hilal Al Sahil ya Sudan kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Septemba 17.

Akizungumza na Spotileo nahodha huyo amesema kilichosababisha kupoteza mchezo wa kwanza Sudan ni kutowajua vizuri wapinzani hao.

“Hilal Al Sahil ni timu nzuri lakini hawana nafasi ya kushinda mechi ya pili, benchi letu la ufundi limetupa mbinu bora za kupata ushindi, kwa hiyo naamini itakuwa zamu yetu kushinda na kutinga hatua inayofuata,” amesema Lyanga.

Mshambuliaji huyo amesema malengo ni kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ya michuano hiyo hivyo Geita itakikisha inafanya juhudi kubwa kushinda mchezo huo.

Amesema pamoja na kupoteza mchezo uliopita timu yake ilicheza vizuri na kuutawala mchezo ingawa makosa madogo yaliyowagharimu na kufungwa bao hilo.

Geita Gold inashiriki kwa mara ya kwanza michuano ya kimataifa tangu kuanzishwa kwake.

Related Articles

Back to top button