Burudani

Gara B awakumbuka vijana sekta ya ushereheshaji

MSHEREHESHAJI Godfrey Deogratius Rugalabamu maarufu ‘Gara B’ amesema ameandaa programu ya ‘Upskills na Gara B’ ambayo itamwezesha kijana wa Kitanzania kuonesha uwezo wake wa kusherehesha.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, Gara B ameiambia SpotiLEO kuwa mpango huo ni kama sehemu ya kurudisha kwa jamii kutokana na kazi anazofanya.

“Inalenga kunyanyua vipaji kwa wale ambao wanahisi wana uwezo wa kuwa washereheshaji lakini ambao wako kwenye ‘field’ kuwaongezea ujuzi, misingi na maadili,” amesema Gara B.

Gara B ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha ‘Mr Right Show’ amesema programu hiyo sio mara ya kwanza kurudisha kwa jamii, amewahi pia kurudisha kwa jamii na atandelea kufanya hivyo.

Related Articles

Back to top button