Kwingineko

Forest yataka historia Europa

NOTTINGHAM: klabu ya Nottingham Forest inalenga kusherehekea mchezo wake wa kwanza nyumbani katika michuano ya Ulaya baada ya takriban miaka 30 kwa ushindi wa kwanza chini ya kocha mpya Ange Postecoglou.

Forest itakabiliana na Midtjylland ya Denmark baadae leo, wiki moja baada ya kuanza kampeni ya Europa League kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Real Betis. ikiwa mara ya kwanza kwa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England kushiriki tena michuano ya Ulaya tangu 1996, ilipofika hatua ya robo fainali ya Kombe la UEFA, mashindano yaliyokuja kubadilishwa jina kuwa Europa League.

“Kuna mashabiki wengi wa Forest ambao hawakuwahi kushuhudia timu yao Ulaya, kwa hiyo itakuwa jambo la kusisimua kwa kila mtu kuona, Ni historia inayoandikwa na tunataka kufanikisha mambo makubwa kupitia hili.” – alisema mshambuliaji Chris Wood.

Forest bado haijashinda katika michezo mitano chini ya Postecoglou, aliyewahi kuinoa Tottenham, tangu achukue nafasi ya Nuno Espírito Santo aliyefutwa kazi.

Katika upande mwingine, klabu nyingine ya England, Aston Villa, inasafiri kwenda Feyenoord ikiwa na morali ya ushindi wake wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu, mabao 3-1 dhidi ya Fulham, baada ya pia kushinda 1-0 dhidi ya Bologna katika mechi ya kwanza ya Europa.

Wawakilishi wa Scotland, Celtic na Rangers, wanatafuta ushindi wao wa kwanza watakapomenyana na Braga na Sturm Graz mtawalia.

Related Articles

Back to top button