Filamu
Filamu ya Priyanka Chopra ‘The Bluff’ yavunja rekodi

INDIA: FILAMU mpya ya muigizaji wa Bollywood Priyanka Chopra iitwayo ‘The Bluff’ imefanikiwa kuwa filamu ya asili iliyotazamwa zaidi katika majukwaa ya utiririshaji (OTT) duniani licha ya kupokea maoni mchanganyiko kutoka kwa wakosoaji.
Filamu hiyo iliyotolewa Februari 25 kwenye jukwaa la Amazon Prime Video, imekusanya takribani dakika milioni 300.3 za watazamaji katika kipindi cha wiki moja tu.
Katika orodha hiyo, filamu ya kusisimua ‘Accused’ inayopatikana kwenye Netflix imefuata katika nafasi ya pili kwa dakika milioni 213.1 za watazamaji.
Filamu nyingine zilizofanikiwa katika orodha hiyo ni pamoja na ‘Firebreak’, ‘Paul McCartney: Man on the Run’, pamoja na ‘The Wrecking Crew’ ambazo pia zimevutia watazamaji wengi duniani.




