Familia

Familia yaweka wazi chanzo cha kifo cha Mtangazaji wa Fox Sports

LOS ANGELES:FAMILIA ya mmoja wa waanzilishi na mtangazaji wa zamani wa kipindi cha Sayansi ya Michezo cha Fox Sports na ESPN, John Brenkus imeweka wazi uchunguzi wa kifo cha ndugu yao huyo.

Kwa mujibu wa familia hiyo uchunguzi wao hauoneshi dalili zozote za matatizo ya afya ya kimwili, ajali, au mchezo mchafu unaochangia kifo cha ndugu yao huyo kutokea.

Familia ya John Brenkus, waliongeza kwamba Brenkus alikuwa akikabiliwa na vita vya muda mrefu na huzuni. Hadi anafariki Mei 31, 2025 alikuwa na umri wa miaka 54.

“Ni kwa huzuni kubwa kwamba tunashiriki habari kwamba John Brenkus ameaga dunia. John, mwanzilishi mwenza wa Base Productions, mwanzilishi wa Brinx.TV, na mtayarishaji mwenza na mtangazaji wa Tuzo za Emmy ya Sayansi ya Michezo iliyoshinda Tuzo la 6, alikuwa akipambana na huzuni. John alishindwa kupambana na ugonjwa huo mbaya akafariki Mei 31, 2025,” taarifa hiyo ilieleza.

Awali familia hiyo iliweka taarifa za kifo cha Brenkus katika mitandao yake ya kijamii na haikutaja chanzo kamili cha kifo chake kilichotokea Mei 31, 2025 huku wengi wakiwa na wasiwasi na chanzo cha kifo cha mtangazaji huyo.

Related Articles

Back to top button