FAILUNA ATAMBA RIADHA TAIFA

FAILUNA Abdi amedhihirisha umwamba wake katika mbio hapa nchini baada ya kushinda mbio za meta 10,000 katika Mashindano ya Taifa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Failuna ambaye amekuwa akitamba katika mbio mbalimbali za nusu marathoni na marathoni nchini, alishinda mbio hizo za jana kwa kutumia muda wa dakika 34:39.17, huku Natalia Sulle wa Kusini Unguja akimaliza wa pili kwa kutumia dakika 35:02.21.
Faiuna mwaka huu alikuwa mwanariadha pekee wa kike kutoka Tanzania aliyeshiriki nichezo ya Olimpiki iliyofanyika Tokyo akikimbia marathoni na kumaliza wa 40 huko Sapporo, Japan.
Mshindi wa tatu ni Maiselina Issa wa Arusha aliyemaliza kwa kutumia dakika 36:47,15 na Angel Yumba alimaliza wa nne kwa 37:10.60 na Neema Nyaisawa wa Mara alimaliza wa nne kwa kutumia dakika 38:57,58,
Katika mbio za meta 800 wanaume, Simon Msonjo wa Kilimanjaro alimaliza wa kwanza kwa kutumia 1:53.14 huku wa pili akiwa ni Steward Mboya wa Arusha aliyetumia dakika 1:54.16 na Damiani Christian wa Kilimanjaro alishika nafasi ya tatu kwa dakika 1:55.90.
Transfora Mussa wa Arusha alitamba katika mbio za meta 5,000 wanawake baada ya kumaliza wa kwanza kwa dakika 17:09.45, Anastazia Dolomongo wa Arusha alimaliza wa pili kwa kutumia dakika 17:13.94 na Natalia Elisante wa Kusini Unguja alipata medali ya shaba kwa dakika 17:30.00.
Katika mbio za meta 800 wanawake, mkoa wa Pwani uliibuka kidedea baada ya mwanariadha wake Regina Mpigachai kumaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 2:12.64, Transfora Mussa wa Arusha alimaluza wa pili kwa kutuia dakika 2:16,36 na Mariam Salum wa Arusha alimaliza wa tatu kwa dakika 2:17.66.
Katika mbio za meta 10,000 kwa wanaume juzi kwenye uwanja huohuo, mwanariadha mwingine wa kimataifa wa Tanzana, Alphonce Simbu alishindwa kutamba baada ya kumaliza watatu huku Faraja Lazaro wa Arusha akishinda.