Elon Musk aitamani Liverpool

BABA yake Elon Musk, Errol Musk amesema kuwa mwanaye bilionea Elon Musk ameonesha nia ya kuinunua klabu ya soka ya Liverpool ya Uingereza.
Klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza inamilikiwa binafsi na Fenway Sports Group (FSG), ambayo haijaonesha dalili za kutaka kuuza lakini imewahi kukubali uwekezaji wa nje hapo awali.
Errol Musk, wakati wa mahojiano na Times Radio, alithibitisha kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla ameonesha shauku kwa klabu hiyo yenye mataji sita ya Kombe la Ulaya.
“Oh ndiyo, lakini hiyo haimaanishi kuwa atanunua,” alisema Errol Musk. “Angependa, ndiyo, bila shaka, kila mtu angependa. Hata mimi pia.”
Hata hivyo, msemaji wa FSG alipohojiwa na Shirika la Habari la Associated Press alisema kuwa “Hakuna ukweli wowote kwa uvumi huu”.
Wana Liverpool, vipi mwana apewe timu?