EPLKwingineko

Disasi ni wa bluu

BEKI wa kimataifa wa Ufaransa Axel Disasi amejiunga na klabu ya Chelsea’The Blues’ akitokea Monaco kwa mkataba wa miaka sita, ada ikiwa Euro milioni 45 sawa na shilingi bilioni 117.49.

Disasi mwenye umri wa miaka 25 anaziba nafasi ya ulinzi Stamford Bridge baada ya Wesley Fofana kupata majeraha ya goti.

Alicheza mechi zote 38 za Monaco Ligue 1 msimu uliopita.

“Kwa kweli najivunia kuwa sehemu ya familia hii kubwa,” amesema Disasi kupitia tovuti ya Chelsea.

Disasi amecheza michezo 129 akiwa Monaco baada ya kujiunga na klabu hiyo Agosti 2020 akitokea Stade de Reims.

Beki huyo wa kati anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa Chelsea majira haya ya joto baada ya Christopher Nkunku, Nicolas Jackson, Lesley Ugochukwu, Angelo Gabriel na Diego Moreira, wakati kocha mpya Mauricio Pochettino akiendelea kuimarisha kikosi.

Related Articles

Back to top button