Nyumbani
Dirisha dogo usajili lafunguliwa

DIRISHA dogo la usajili kwa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara limefunguliwa leo na litafungwa Januari 15, 2023.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imesema klabu zinatakiwa kutumia kipindi hicho kufanya usajili na kukamilisha uhamisho.
TFF imesema baada ya kufungwa kwa dirisha hakutakuwa na muda wa zaida hivyo ni vyema klabu zikakamilisha usajili na uhamisho kwa wakati.
Taarifa hiyo imesema klabu itakayokutana na changamoto yoyote wakati wa usajili iwasiliane na Idara ya mashindano TFF.