Mastaa

Diamond: Wanamuziki wameanza kupewa thamani 

DAR ES SALAAM:MWANAMUZIKI Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema kitendo cha serikali kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji yamesaidia kampuni mbalimbali kuwatumia wasanii kama mabalozi wa bidhaa na kuwaheshimisha.

Kauli yake hiyo inakuja baada ya kampuni ya Pepsi Tanzania (SBC) kutangaza kuendeleza ushirikiano wa kibiashara na msanii huyo huu ukiwa nim waka wa saba wanafanya kazi Pamoja.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo Diamond amesema kitendo cha kampuni hiyo kumtumia mwanamuziki kuwa balozi wao ni kitu cha heshima inaonesha kwamba wanamuziki wameanza kupewa thamani, wanapendwa, wanakubalika na kuthaminika.

“Naipongeza serikali kwasababu wameweka miundombinu rahisi inayowezesha hivi vyote kukamilika kwasababu wasingeweka hivyo pengine ingekuwa ngumu,

“Ni heshima kwa taifa kuonekana kwamba nchi hii haina wanamuziki wa hovyo kwasababu zamani walikuwa wanachukuliwa mastaa kutoka nje, picha zao zinatumika lakini sasa hivi tunatumika hapa Tanzania maana yake kama wanamuziki, waandishi wa Habari nan chi tumefanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba chapa zetu za kimuziki zina thamani zinaweza kushirikiana na taasisi kubwa kama hizi,”aliongeza.

Alisema ushirikiano wao umemsaidia kuongeza thamani yak na ya bidhaa husika. “Niwashukuru Pepsi nimefanya nao kazi kuanzia 2018 mpaka sasa na toka tumeanza kufanya Kazi, tumekuwa tukifanya kazi kwa mafaniko hii inaonesha ni kampuni sahihi,”

Meneja Masoko wa SBC Tanzania Jasper Maston alisema ushirikiano huu na Diamond Platnumz unaakisi kile wanachokiamini kuhusu chapa ya Pepsi kuwa kinywaji baridi cha ubunifu, cha vijana, na cha kitani.

Amesema ushirikiano huo utamhusisha Diamond katika shughuli zake zote za muziki ikiwemo matangazo, matamasha ikiwemo Wasafi na shughuli nyingine za kijamii.

“Diamond anawakilisha ujasiri na uhalisia ambao Pepsi inasimamia, uhusiano wake na watu pamoja na ubunifu wake usioyumba, unalingana na dhamira yetu ya kuwa na umuhimu na matarajio, kwa mashabiki upendo wenu unatuhamasisha. Tunamshukuru Diamond kwa kuwa Pamoja nasi”aliongeza.

Related Articles

Back to top button