CHAN

Dar wapewa somo kuelekea CHAN

DAR ES SALAAM;  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametoa wito kwa taasisi na wadau wote kuhakikisha maandalizi mazuri ya miundombinu hasa barabara, usafi wa mazingira, hoteli inakuwa vizuri wakati huu wa kuelekea kwenye michuano ya CHAN inayotarajia kuanza mwezi ujao.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Chalamila amesema kutakuwa na wageni wengi kwenye michuano hiyo na kwamba hiyo ni fursa nzuri kwa Watanzania.

Michuano ya CHAN inatarajiwa kufanyika mwezi ujao Dar es Salaam, Zanzibar, Kampala na Nairobi, ambapo timu ya Taifa ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imepangwa kundi moja na timu za Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

“Tunapaswa kuweka miundombinu bora ili wageni waje na wananchi waendelee na kazi zao kama kawaida. Kikubwa ni kuhakikisha barabara zetu na mazingira yanakuwa ya kiwango cha juu,” amesema.

Related Articles

Back to top button