Kwingineko
Dani Alves kuachiwa kwa dhamana

MAHAKAMA ya Hispania imeamua kwamba mchezaji wa zamani wa Barcelona na Brazil Dani Alves anaweza kuachiwa kwa masharti toka jela baada ya kutumikia karibu robo ya kifungo cha mashitaka ya ubakaji.
Alves, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu gerezani mwezi uliopita ataachiwa kwa dhamana ya pauni 853,000.
Amekuwa kwenye kizuizi kabla ya hukumu tangu Januari 2023.
Alves mwenye umri wa miaka 40 alipatikana na hatia ya kosa la kumbaka mwanamke kwenye klabu ya usiku jijini Barcelona Desemba 2022.
Masharti ya kuachiwa ni pamoja na kukabidhi pasipoti za kusafiria za Brazil na Hispania ili asiondoke Hispania.
Pia ni lazima aripoti mahakmani kila wiki.