CV ya kocha mpya Singida inatisha

SINGIDA: UONGOZI wa timu ya Singida Black Stars umemtambulisha Kocha Mkuu mpya wa kukinoa kikosi cha timu hiyo , Hamdi Miloud kutoka nchini Ufaransa amechukuwa nafasi ya Patrick Aussems.
Hamadi mwenye leseni ya ukocha wa daraja la UEFA A anapendelea kutumia mfumo wa 4-2-3-1 ana uzoefu wa soka la Afrika kwa kuzinoa klabu mbalimbali zikiwemo USM Alger na JS Kabyile za Algeria, Al- Salmiya ya Kuwait, TP Mazembe ya Congo, Athletico Marseille na ES Vitrolles za Ufaransa na Al- Ettifaq FC ya Saudia Arabia.
Taarifa kutoka kwa Ofisa Habari wa Singida Black Stars, Hussein Massanza kuwa Hamadi amekuja kuchukuwa nafasi ya Aussems baada ya kuondolewa kutokana na kutokuwa na matokeo mazuri.
Massanza amesema Hamadi atasaidiwa na makocha wasaidizi wawili; Kocha Nassim Anisse na Kocha David Ouma.
“Tumefanya mchakato wa kutafuta kocha kwa kipindi kirefu, tumefanikiwa kumpata Hamadi tumeridhishwa na wasifu wake tunatarajia atatusaidia kufikia malengo yete kwenye michezo iliyosalia ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la CRBD ” amesema.
Massanza amesema Kocha Hamdi ana rekodi nzuri ya kufika Hatua ya Fainali katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League – Finals), Robo Fainali mara mbili Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL Quarter Finals) na Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC Quarter Finals)
Massanza amesema aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu, Ramadhani Nsanzurwimo, amerejea kwenye majukumu yake kama Mkurugenzi wa Ufundi.