
LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Coastal Union inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 7 baada ya michezo 6 wakati Geita Gold inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 6 baada ya michezo 6 pia.
Kwa mara ya mwisho timu hizo zilikutana Juni 29, 2022 katika mchezo wa Ligi Kuu huku matokeo yakiwa sare ya bao 1-1.