FANyumbani

Coastal kuitoa Simba ASFC leo?

MICHUANO ya Kombe la Shikisho la Azam(ASFC) hatua ya raundi ya tatu inaendelea leo michezo sita ikipigwa kwenye viwanja tofauti.

Wekundu wa Msimbazi, Simba itakuwa wenyeji wa washirika wao wagosi wa kaya, Coastal Union kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Katika michezo mingine KMC itavaana na Copco kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati New Dundee ni wenyeji wa African Sports kwenye uwanja wa Jamhuri.

Mbeya City ni wageni wa Mbeya Kwanza kwenye uwanja wa Majimaji, Songea wakati Singida Big Stars itaikaribisha Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Liti, Singida.

Nao matajiri wa dhahabu, Geita Gold itakuwa mwenyeji wa Nzega United kwenye uwanja wa Nyankumbu uliopo Halmashauri ya Geita.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button