EPL

“City itarudi imara” – Al Mubarak

MANCHESTER: MWENYEKITI wa mabingwa wa Ligi Kuu ya England mara nne mfululizo Manchester City Khaldoon Al Mubarak amesema klabu hiyo itarejea kwenye ubora wake akituma salamu kwa washindani wao kuwa ya msimu huu yameisha na wajiandae kuipokea City tofauti msimu ujao ambapo tayari wameanza hekaheka kuelekea msimu huo.

Al Mubarak ameyasema hayo katika mahojiano yake ya kila mwisho wa msimu ambapo amekuwa na kawaida ya kuzungumzia msimu unaomalizika na maandalizi ya kuelekea msimu mpya wakianza na Kombe la Dunia la Klabu la Katikati ya mwezi Ujao akikiri kuteleza msimu.

“Tutarudi, Msimu huu ni msimu ambao sasa uko nyuma yetu. Leo ni siku mpya. Tunaanza kufanya kazi ya kujiandaa kwa msimu ujao, tumekuwa tukifanya hivyo tangu Januari. Na tutahakikisha mambo yote mazuri na yasiyo mazuri ya msimu huu tumeyachukua na kujifunza kutoka kwayo na kujiboresha na kuwa bora zaidi”.

“Na niwahakikishie, Klabu hii itafanya kila liwezekanalo kurejea katika viwango ambavyo tunajua sote tunaweza kufikia na tunachojua, tutafikia. Kwa sababu kusema kweli, kama kuna jambo ambalo ningependa kwa sasa, ni kufunika ukurasa huu mbaya wa msimu uliopita na kuanza mara moja kuzingatia msimu ujao.” – alisema

Manchester city hawajawa na msimu mzuri ukizingatia mafanikio yasiyo na kifani katika miaka ya hivi majuzi, kwa kutwaa mataji matatu (treble) ya msimu wa 2022/23 ikifuatiwa na kukamilisha rekodi ya mataji manne ya Ligi Kuu ya Uingereza, msimu huu City walimaliza na Ngao ya Jamii pekee.

Related Articles

Back to top button