Chris Brown afichua tabia yake ya siri anapokuwa safari

MAREKANI:STAA wa muziki duniani, Chris Brown, amefichua tabia yake ya kipekee anapokuwa kwenye miji tofauti kwa ajili ya shows au mapumziko.
Chris anasema huwa anapenda “kutoroka peke yake usiku” ili kutembea mitaani kama mtu wa kawaida.
Kwa mujibu wa msanii huyo, kutembea akiwa peke yake kunampa utulivu wa akili na kumfanya ajisikie huru.
“Ninapenda kutoroka peke yangu ninapokuwa miji tofauti. Inanisaidia kujisikia binadamu wa kawaida, hiyo ni muhimu sana kwa akili yangu kutokana na siwezi kutembea kwa uhuru wakati wa mchana,” amesema Chris Brown.
Kwa nyota kama Chris Brown ambaye maisha yao yanafuatwa kila kona, hii ni njia ya kupumzisha akili na kuishi kama ‘mtu wa kawaida’, hata kwa muda mfupi.
Maoni yako je? Unaona ni njia nzuri ya kukabiliana na presha ya umaarufu au kuna hatari zake?