Tetesi

Chelsea yamwinda Cole Palmer

KLABU ya Chelsea ‘The Blues’ ya Kaskazini ya London imeonesha nia kumsajili fowadi wa Manchester City na timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, Cole Palmer.

Inafahamika kuwa hakuna ofa rasmi iliyowasilishwa.

Kocha Mauricio Pochettino amesema The Blues inaweza kumsajili mchezaji mmoja zaidi wa eneo la kiungo kipindi hiki cha dirisha la uhamisho, lakini amesisitiza kuwa usajili mpya lazimia uendane na mahitaji ya timu.

Palmer mwenye umri wa miaka 21 anaweza kucheza nafasi mbalimbali kwenye safu za ushambuliaji na kiungo.

Siku zilizopita Kocha wa City, Pep Guardiola, alisema Palmer hataruhusiwa kuondoka kwa mkopo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button