Ligi Ya WanawakeNyumbani

Ceasiaa vs The Tiger kivumbi wanawake leo

KLABU ya The Tiger Queens leo itakuwa mgeni wa Ceasiaa Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka ya Wanawake Tanzania Bara.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Mkwawa mkoani Iringa.

Ceasiaa Queens inashika nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 3 baada ya michezo 4 wakati The Tiger Queens ipo nafasi ya 9 ikikusanya pointi 1 baada ya michezo 3.

Mchezo mmoja wa ligi hiyo umepigwa Januari 12 ambapo wenyeji Baobab Queens imeshindwa kutumia uwanja wake wa nyumbani wa Jamhuri jijini Dodoma baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga Princess.

Related Articles

Back to top button