Kwingineko

“Caicedo ni mzalendo wa kweli” – Maresca

EAST RUTHERFORD, Kiungo wa kati wa Chelsea, Moisés Caicedo aliumia kifundo cha mguu wake wa kushoto dakika za nyongeza za kipindi cha pili katika ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Fluminense kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia la Klabu kabla ya kutolewa kwa matibabu na Chelsea kumaliza mchezo huo pungufu.

Baada ya kuumia Caicedo alipata matibabu uwanjani na akarejea kwenye mchezo kisha kutolewa baadae kidogo kwa matibabu zaidi huku Chelsea ikimaliza pungufu ya mchezaji mmoja.

Kocha wake Chelsea Enzo Maresca amesifu uzalendo wa kiungo huyo kwani alijua mapema kama alikuwa ameumia lakini alitaka ajikaze na kumalizia mchezo kwa dakika zilizosalia kabla ya kushindwa kuendelea na kutoka kwa matibabu zaidi alipoona wanaweza kumaliza mchezo na ushindi.

“Moisés, aliumia kifundo cha mguu mapema lakini nilimwambia kwa sababu zimesalia dakika mbili, tatu hivi, tunaweza kucheza na wachezaji 10 apumzike. Jambo muhimu ni kwamba haikuwa inazidi kuwa mbaya, kwa sababu tuna mechi Jumapili”

“Lakini kijana huyu aliona kwamba angeweza kujaribu kumaliza mchezo. Akajaribu lakini alihisi maumivu makali na akashindwa kuendelea. Tunamuombea, tunatumai anaweza kuwa fiti Jumapili.” meneja wa Chelsea Enzo Maresca amesema

Chelsea inacheza na Real Madrid au Paris Saint-Germain katika fainali ya Kombe la Dunia la Klabu Jumapili. Huku kukiwa na sintofahamu kama Moisés Caicedo ataweza kuwepo katika mchezo huo.

Related Articles

Back to top button