Muziki

Burna Boy atamani kutumbuiza Bure Burkina Faso

MSANII maarufu wa Nigeria na mshindi wa tuzo mbalimbali, Burna Boy, ametangaza nia ya kufanya tamasha la bure nchini Burkina Faso kama ishara ya heshima kwa Rais Ibrahim Traoré na watu wa taifa hilo.

Kupitia Insta Story yake, Burna Boy aliandika kwa hisia: “Ikiwezekana, itakuwa heshima kwangu kuwapa watu wa Burkina Faso tamasha la bure la Burna Boy wakati fulani mwaka huu, Insha Allah.”

Ujumbe huo umeibua msisimko mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo mashabiki na wanaharakati wa Pan-African wamesifu hatua hiyo kama ishara ya upendo wa bara moja na ukarimu wa hali ya juu wa kisanii.

Iwapo tamasha hilo litatimia, litakuwa tukio la kihistoria katika tasnia ya burudani ya Burkina Faso, na kuwapa wananchi wake fursa ya kipekee ya kufurahia burudani ya kiwango cha kimataifa bila malipo – chini ya mwanga wa mshikamano na heshima kwa Rais Ibrahim Traoré.

Related Articles

Back to top button