EPLKwingineko

Brighton yamsajili Ansu Fati kwa mkopo

MSHAMBULIAJI wa Hispania Ansu Fati amekamilisha uhamisho kwenda Brighton & Hove Albion ya England kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Barcelona.

Ripoti zimesema dili la Fati mwenye umri wa miaka 20 halihusishi sharti la kumnunua.

“Hili ni dili kubwa kwetu sote. Nina hakika Ansu atatusaidia kufikia malengo mapya na tunaweza kumsaidia kurejea kwenye kiwango chake anachostahili kuwa,” amesema Kocha wa Brighton Roberto De Zerbi.

Brighton itashriki michuano ya ulaya msimu huu kwa mara ya kwanza baada ya kufuzu Ligi ya Europa ikiwa kundi B pamoja na Ajax ya Uholanzi, Marseille ya Ufaransa na AEK Athens ya Ugiriki.

Brighton italipa asilimia 80% ya mkataba wa Fati kufikia mwisho wa Juni, 2024. Gharama ya jumla ya mishahara ni karibu pauni milioni 7 sawa na shilingi bilioni 21.6.

Septemba 2019, Fati alikuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi wa Barcelona kuwahi kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na goli lake dhidi ya Inter Milan Desemba 2019 lilimfanya kuwa mfungaji mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na miaka 17 na siku 40.

Related Articles

Back to top button