Kwingineko

Brazil kujipima na Korea Kusini, Japan

BRAZIL: TIMU ya soka ya Brazil itacheza mechi za kirafiki mwezi Oktoba huko Korea Kusini na Japan huku timu zote tatu zikiwa katika maandalizi ya Kombe la Dunia la mwaka 2026.

Ikifundishwa na Muitaliano Carlo Ancelotti, Brazil inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo itakayofanyika mwakani nchini Marekani, Canada na Mexico.

Wenyeji Brazil walizuru Korea Kusini mara ya mwisho kwa mechi ya kirafiki mnamo Juni 2022, kabla ya Kombe la Dunia la Qatar, na walishinda 5-1 huku Neymar akifunga mara mbili kwa mkwaju wa penalti.

Vijana wa Ancelotti kisha watacheza na Japan kwenye Uwanja wa Tokyo, ambao una uwezo wa kuchukua watu chini ya 50,000, Oktoba 14, FA ya Japan imeeleza.

Neymar mwenye umri wa miaka 33 hajavaa jezi ya Brazil kwa takriban miaka miwili kwa sababu ya majeraha ya mara kwa mara na hakuingia kwenye kikosi cha sasa cha Ancelotti.

Related Articles

Back to top button