Brad Pitt yuko tayari kufanya kazi na Tom Cruise kwa masharti

LOS ANGELES: MCHEZA filamu Brad Pitt, ambaye anakodolea macho kuachiliwa kwa drama yake ya michezo ya magari Formula One ‘F1: The Movie’, amefunguka juu ya uwezekano wa kushiriki na mcheza filamu mwenzake Tom Cruise lakini kwa sharti moja.
Wawili hao walionekana pamoja katika Mahojiano ya filamu ya 1994 na ‘Vampire’. Katika mahojiano, Pitt alisema angependa kufanya kazi na Tom Cruise, lakini kwa sharti moja kwamba hataki masuala ya kuruka angali kama filamu nyingi za Tom Cruise zinavyofanya.
“Kwa sasa nashughulika na filamu ya F1, lakini mambo ya kuninginiza mwili wangu sitaki hilo ndilo sharti kubwa ili niweze kushiriki filamu pamoja na Ton Cruise,” amesema Brad Pitt.
Hapo awali, Pitt na Cruise walishirikiana kwa filamu ya 1994, iliyoitwa Mahojiano na ‘Vampire’.
Wakati huo huo, mapema mwaka huu katika hafla ya Paramount, Tom Cruise alisifu ustadi wa kuendesha gari wa Brad Pitt, haswa kutokana na filamu yake ijayo ya F1.
Filamu ya F1: Imeongozwa na Joseph Kosinski. Bingwa wa Formula 1 na dereva Muingereza Lewis Hamilton ameunga mkono filamu hiyo inayotarajiwa kutoka Juni 27 ikiwa na baadhi ya waigizaji Damson Idris, Javier Bardem na Kerry Condon.