Mastaa

Binti afichua kifo cha Baba yake Val Kilmer

NEW YORK: STAA wa Hollywood Val Kilmer amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65 huku Binti yake Mercedes Kilmer akithibitisha kuwa ugonjwa wa nimonia ndiyo uliosababisha kifo cha baba yake.

Kilmer aliyehusika kwa mafanikio katika filamu ya ‘Top Gun’ na ‘Batman Forever’ (1995), aligundulika kuwa na saratani ya koo mwaka wa 2014.

Katika taarifa yake kwa gazeti la The New York Times, binti huyo amesema nimonia ndiyo iliyosababisha kifo cha baba yake huku akidai saratani ya koo aliyokutwa nayo mwaka 2014 ilipona kabisa.

Kilmer alifanya filamu yake ya kwanza katika filamu ya kipelelezi mwaka 1984 na akaonyesha mbwembwe zake za vichekesho katika filamu ya ‘Real Genius’ (1985), amecheza kama mwanajeshi wa ndege Tom kwenye filamu ya ‘Iceman’.

Filamu nyingine alizocheza ni ‘Top Gun’, ‘Howard Willow’ (1988) na ‘The Doors’ (1991).

Kilmer alipatikana na saratani ya koo mwaka wa 2014. Val, filamu ya hali halisi kuhusu maisha yake iliyooneshwa kwa mara ya kwanza huko Cannes Julai 2021, ilimwonesha akihitaji bomba la kupumua.

Katika ripoti hiyo, binti yake alisisitiza kuwa Val aligunduliwa na saratani ya koo mnamo 2014 na akapona.

Ndoa ya Val na mwigizaji Joanne Whalley, ambaye aliweka kwenye seti ya filamu ya fantasia ya watoto ya Ron Howard Willow (1988), ilimalizika kwa talaka. Walionusurika ni pamoja na watoto wao, Mercedes na Jack. Val aliishi kwenye shamba karibu na Santa Fe kwa miaka mingi.

Related Articles

Back to top button