
TIMU ya Azam imetangaza kuachana na makocha wawili katika benchi la ufundi la timu kati.
Kwa mujibu wa taarifa ya Azam, iliyowatema ni Kocha wa magolikipa Dani Cadena na wa viungo Dk Moadh Hiraoui.
“Ahsanteni sana kwa utumishi wenu mzuri ndani ya klabu yetu. Tunawatakia kila la kheri katika safari yenu mpya ya ukocha popote muendapo,”imesema Azam.
Azam haijaeleza watakaochukua nafasi zao.