Azam ugenini shirikisho Afrika

KLABU ya Azam leo itakuwa ugenini Libya kuikabili Al Akhdar katika mchezo wa raundi ya pili Kombe la Shirikisho Afrika katika uwanja wa Benina Martyrs ulipo mji wa Benghazi.
Mchezo huo ni miongoni mwa mechi 9 za michuano hiyo zinazopigwa leo.
Awali akizungumza na Spotileo Mtendaji Mkuu wa Azam Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema klabu hiyo imejipanga vyema kuhakikisha inapata ushindi dhidi ya Al Akhadar.
Popat amesema malengo ni kufika mbali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika angalau hatua ya makundi hivyo wamezungumza na wachezaji na wanaamini watapata matokeo mazuri.
“Tumefika salama na tunawashukuru wenzetu Al Akhdar wametupa mapokezi mazuri na wachezaji wetu wanaonekana wana ari kubwa ni imani ya kila mmoja wetu kwamba tutapata matokeo mazuri kesho,” amesema Popat.
Amesema wachezaji wapo katika hali nzuri kwa ajili ya mechi hiyo.
Michezo mingine inayopigwa leo ni kama ifuatavyo:
St Michel United vs Motema Pembe
AS Kigali vs Al-Nasr
Ferroviario da Beira vs Diables Noirs
Kipanga vs Club Africain
Saint-Eloi Lupopo vs Sagrada Esperance
Sporting Gagnoa vs JS Saoura
Al Hilal Wau vs Pyramids
AS Real Bamako vs Hearts of Oak