Nyumbani

Azam FC ‘yatema’ rasmi wanne

DAR ES SALAAM: KLABU ya Azam FC imewaaga rasmi wachezaji wake wanne waliokuwa sehemu ya kikosi chake msimu uliopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo leo, Azam FC imewashukuru kwa huduma ya nyota hao ikiwemo Jhonier Blanco, Mamadou Samake, Franck Tiesse na Ever Meza, huku ikiwatakia mafanikio mema katika safari zao mpya za soka.

“Nawashukuru nyote kwa huduma na nawatakia kila la heri,” ilisomeka taarifa ya klabu, ikionesha kuthamini mchango wa wachezaji hao waliokuwa sehemu ya kikosi kilichoshindana kwenye Ligi Kuu ya NBC na michuano mingine ya ndani.

Uongozi wa Azam FC umeeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mabadiliko na maandalizi ya kikosi kipya kwa msimu ujao, ambacho kinatarajiwa kuwa na uso mpya na ushindani mkubwa zaidi.

Blanco alijiunga na Azam FC mwaka jana akitokea Aguilas Doradas ya Ligi Kuu Colombia. Samake na Tiesse na Meza pia walijiunga msimu uliopita na wachezaji hao walitajwa wangeondoka mapema kwani Kocha Mkuu Frorent Ibenge hana mpango wao.

Related Articles

Back to top button