Azam FC yataka makundi shirikisho

GIZA: MAKAMU wa Rais wa Azam FC, Abdulkarim Amin maarufu ‘Popat’ amesema lengo la kwanza la timu hiyo katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu ni kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo.
Timu hiyo iko Misri kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ZED FC utakaochezwa kesho.
Popat amesema: “Azam FC imejipanga kufanya vizuri katika mashindano hayo baada ya msimu uliopita kufanikiwa kufika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu yetu, baada ya hapo ndipo tutafikiria malengo mengine,”
Amesema baada ya kufuzu hatua hiyo, malengo ya timu yatapanuka kulingana na hatua itakayofikia, huku akieleza kuwa viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wameungana kuhakikisha wanafikia lengo hilo.
Wapinzani wa Azam ZED ni miongoni mwa timu ambazo sio maarufu ila zinajitahidi kufanya vizuri kwenye ligi ya Misri ambapo kwa sasa iko katika nafasi ya 10 kwa point inane.




