Ayra Starr ashangazwa na wimbo wake mpya ‘All The Love’ Na Festo Polea

LAGOS : WIMBO Mpya wa kwanza kwa mwaka huu 2025 wa mwanamuziki na mtunzi wa nyimbo mbalimbali Ayra Starr ‘All the Love’ aliouachia siku tatu zilizopita umeanza kufanya vizuri nchini Nigeria na nchi za karibu kutokana na ujumbe uliopo katika wimbo huo.
Nyota huyo wa Nigeria ameachia single hiyo akiwa na lengo la kuashiria sura mpya baada ya albamu yake ya pili iliyosifika zaidi ya ‘The Year I Turned 21’ lakini mapokezi ya wimbo huo yamemshangaza hadi mwenyewe.
Ayra amesema: “Nilirekodi wimbo huu nikiwa najipenda, na ninatumai mashabiki wangu wanahisi vivyo hivyo, nami,”
Ayra ameendelea kufanya vizuri ambapo hivi karibuni alikamilisha ziara yake ya ‘Coldplay’ huko Australia na New Zealand, huku wimbo wake wa ‘Rush’ ukipakuliwa na watu bilioni 1 kote duniani. Amewahi kuchaguliwa katika Tuzo za Burudani za Kiafrika za 2024 huko Marekani ambapo alishinda tuzo ya Msanii Bora wa Kike kwa Jumla barani Afrika na Msanii Bora wa Kike Afrika ya Kati na Magharibi.
Tangu mwaka wake wa kwanza wa 2021, Ayra amepanda umaarufu duniani kwa vibao bora zaidi na teuzi nyingi za VMA. Wimbo wake wa ‘Rush’ ulimfanya kuwa msanii wa kike mwenye umri mdogo zaidi barani Afrika kutazamwa na zaidi ya watu milioni 100 kwenye YouTube.
Mnamo 2023, alikua mteule mdogo zaidi katika tuzo za Grammy, kupanda kwa Ayra Starr kunaendelea kutangaza vyema muziki wa Nigeria na Afrika kwa ujumla.




