Europa

Aston Villa mwendo mdundo UEL

BASEL: WABABE wa Arsenal, Aston Villa wameendeleza mwendo mzuri kwenye UEFA Europa League (UEL) baada ya kuishushia kipigo cha mabao 2-1 kwa FC Basel ya Switzerland, Alhamisi usiku, kupitia mabao ya Evann Guessand na Youri Tielemans.

Ushindi huo umeifikisha Villa kwenye pointi 15, sawa na vinara wa ligi hiyo Olympique Lyonnais na Midtjylland walio nafasi ya pili, wote wakiwa katika nafasi hizo baada ya mechi sita. Basel wamesalia na pointi 6, nje ya nafasi za mtoano.

Villa ilianza mchezo kwa kasi na kufungua ukurasa wa mabao dakika ya 12, baada ya mpira wa kona kuangukia vizuri kwa Guessand aliyemalizia kwa urahisi akiwa umbali mfupi na lango.

Basel walitulia taratibu na kusawazisha dakika ya 34 kupitia Flavius Daniliuc, akiunganisha kwa utulivu krosi ya mpira wa adhabu iliyopangwa vyema na Xherdan Shaqiri.

Baada ya kuingia kutoka benchi, Tielemans alirejesha uongozi kwa Villa dakika ya 53 kwa kumalizia kwa utulivu, kuanzia hapo, Aston Villa walidhibiti mchezo hadi mwisho na kuchota pointi zote tatu ugenini.

Related Articles

Back to top button