EPL

Arteta amsifu Gyökeres licha ya kusuasua kufunga

ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amemsifu mshambuliaji wake Viktor Gyökeres kwa kuonesha juhudi na dhamira kubwa licha ya kukabiliwa na changamoto ya kufunga katika msimu huu.

Arteta amesema mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden anaonesha ari na uvumilivu mkubwa katika harakati zake za kurejesha makali ya ufungaji, huku akiendelea kupambana kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.

Gyökeres mwenye umri wa miaka 28, amekuwa akipata nafasi chache katika hatua za mwanzo za msimu huu na bado hajafunga bao katika mashindano yoyote akiwa na Arsenal, licha ya kuendelea kufanya vizuri katika ufungaji akiwa na timu ya taifa ya Sweden.

Hali hiyo imemfanya mshambuliaji huyo kuwa nyuma katika chaguo la Arteta, ambaye amekuwa akimchezasha Kai Havertz wa Ujerumani kuongoza safu ya ushambuliaji.

Kutokana na hali hiyo, Gyökeres bado hajaanza mchezo wowote wa Ligi Kuu England msimu huu, jambo linalompa changamoto ya kupambana ili kurejesha nafasi yake katika kikosi cha kwanza.

Hata hivyo, Arteta ameonesha imani na mshambuliaji huyo, akisisitiza kuwa dhamira na kujituma kwake ni mambo muhimu katika kipindi hiki anachotafuta kufungua akaunti yake ya mabao akiwa na Arsenal.

Related Articles

Back to top button