Kwingineko

Arsenal yaleta neema Premier League

LONDON: SASA ni rasmi, Ligi Kuu ya England (Premier League) itawakilishwa na timu 5 kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu wa 2025/26 baada ya ushindi wa mabao 3-0 wa Arsenal dhidi ya mabingwa watetezi, Real Madrid, katika mkondo wa kwanza wa michezo ya robo fainali ya ligi hiyo.

Klabu za Uingereza zilihitaji ushindi mmoja tu katika michuano mitatu inayosimamiwa na UEFA ili kujihakikishia nafasi moja kati ya mbili za ziada zinazotolewa kwa mataifa wanachama wa UEFA walioshika nafasi za juu za ubora kwenye viwango vya shirikisho hilo.

Katika mfumo huu, timu hupata pointi mbili kwa kila ushindi kwenye michuano ya Ulaya na pointi moja kwa sare, na jumla ya pointi zote zinazopatikana kwa kila klabu zinagawanywa kwa idadi ya klabu kutoka ligi husika inayoshiriki michuano ya Ulaya.

England inaweza kuwa na hadi timu saba katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao ikiwa Aston Villa itatwaa ubingwa bila kufuzu kupitia msimamo wa ligi kuu, na ikiwa Manchester United au Tottenham Hotspur watabeba makombe ya Europa League na UEFA Conference League.

Vinara wa Ligi, Liverpool na Arsenal wanaoshika nafasi ya pili, wanatarajiwa kuzipata nafasi mbili kati ya tano, huku Nottingham Forest wakishikilia nafasi ya tatu. Chelsea, Newcastle United, Manchester City, Aston Villa, Brighton & Hove Albion, na Bournemouth iliyo nafasi ya 10 wanapambana kwa nafasi hizo kwani tofauti yao ni pointi nane pekee.

Related Articles

Back to top button