EPLKwingineko
Arsenal vs Man City mechi ya mtego EPL

MCHEZO wa kiporo wa Ligi Kuu ya England (EPL) kati ya Arsenal na Manchester City unapigwa leo huku mashabiki wa soka wakisubiri kuona timu ipi itaibuka mbabe.
Kipute hicho pekee cha EPL leo kitachezeshwa na mwamuzi wa kati Anthony Taylor kwenye uwanja wa nyumbani wa Arsenal, Emirates.
Arsenal inaongoza EPL ikiwa na pointi 51 baada ya michezo 21 wakati Man City ina pointi 48 baada ya michezo 22.
Ushindi kwa Arsenal kutaimarisha zaidi nafasi yake kileleni mwa msimamo lakini iwapo Man City itashinda itakuwa sawa kwa pointi na washika bunduki hao wa London kwa pointi 51 huku Arsenal ikiwa nyumba kwa mchezo mmoja.