Amber Lulu aanza kuuza mboga mboga

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva, Amber Lulu, ameibuka na kufichua kuwa kwa sasa ameanza biashara ya kuuza mboga mboga ikiwemo mchicha, matembele na kisamvu ili kujikimu kimaisha.
Akizungumza na Spoti Leo, Amber Lulu alisema hali ya maisha imekuwa ngumu, hivyo ameamua kutafuta mbinu mbadala ya kujipatia kipato licha ya changamoto mbalimbali anazopitia.
“Kuna sit uation napitia lakini sijakata tamaa. Nauza mchicha, matembele mtaani kwa sababu bado naamini nitaweza na sitakata tamaa,” amesema.
Amber Lulu aliongeza kuwa licha ya kuwa msanii anayejulikana, bado anaamini ana nafasi ya kufanikiwa zaidi kama watu maarufu wengine.

“Nilitakiwa kuwa kama watu maarufu wengine lakini bado naamini nitafika. Kufulia ni sehemu ya maisha, na anayenguka lazima asimame. Niwaombe Watanzania mnionee huruma,” amesema.
Amesema biashara hiyo inalenga kumsaidia kujikimu huku akiwaomba watu wenye uwezo wa kifedha kumuunga mkono.
“Ndo maana nafanya biashara ili wenye pesa mje kuni-support na na mimi nipate pesa.”
Katika mahojiano hayo, msanii huyo pia aligusia changamoto za maisha yake binafsi, akieleza kuwa anajutia uhusiano aliokuwa nao na mwanaume aliyemzalia.
“Kit u ninachojutia ni kumzalia mwanaume asiyejua thamani yangu. Sikujua kama hana thamani ya mwanamke. Sijutii kuwa na mtoto, nampenda sana mwanangu kuliko kitu chochote, ila namchukia niliyemzaa naye,” amesema kwa uchungu.




