Albamu mpya ya Katy Perry ‘143’ kutoka Septemba 20

MAREKANI: NYOTA wa muziki nchini Marekani, Katy Perry ameweka wazi kuachia albamu yake anayoiita ‘143’ Septemba 20 mwaka huu.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 ametoa tangazo hilo kwenye mitandao ya kijamii alipokuwa akijiandaa kwa ajili ya uzinduzi wa wimbo wa ‘Woman’s World’.
Jina la ‘143’ ni alama ya wimbo wa ‘I love you’ ambao aliutumia katika jumbe zake alizozituma mara kwa mara katika kurasa zake miaka ya 1990 ambazo zilikuwa zikielezea kuhusu mapenzi na maisha.
“Nilidhamiria kuandaa albamu ya dansi na pop ambayo itakuwa na nyimbo za kuchezeka, kufurahia Maisha yenye ishara 143 za maneno ya upendo kama ujumbe wa moja kwa moja niliokuwa nikiandika.” Katy alisema.
Mkali huyo wa ‘I Kissed A Girl’ ameweka video ya wimbo wake wa ‘Woman’s World’ ikiwa kama kivutio cha albamu yake hiyo anayotaraji kuizindua mwezi Septemba ambapo lich ya wimbo huo ameleza namna ambavyo amekuwa na vibao vingi zilizofanya vizuri kipindi cha nyuma.