Kwingineko

Akothee ahuzunishwa matokeo maandamano ya Gen Z

NAIROBI: MWIMBAJI wa Kenya ambaye pia ni mfanyabiashara Esther Akoth, almaarufu Akothee, amelaani matokeo baada ya maandamano ya SabaSaba yaliyoongozwa na vijana wa Gen Z nchini Kenya.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Akothee ameonesha huzuni yake akidai idadi ya vijana wa Kenya waliojeruhiwa au kuuawa wakati wa maandamano hayo yameongezeka tangu Julai 7, 2025.

“Ni wangapi zaidi wanapaswa kufa kabla ya kusikilizwa?” Akothee alihoji, akiitaka serikali na vyombo vya usalama kuheshimu haki za raia na kuwalinda badala ya kuwadhuru wanaoeleza changamoto zao kwa serikali.

Maandamano hayo, yaliyochochewa na hasira ya umma kuhusu Mswada wa Fedha wa 2024 ulioondolewa na yalibadilika na kuwa hitaji la uwajibikaji wa serikali, haki ya kiuchumi na kukomesha ghasia za polisi.

Katika ombi lake, Akothee alisisitiza ujasiri wa vijana kutetea mustakabali wao:
“Hawa ni watoto wetu. Ndugu zetu. Dada zetu. Maisha yetu ya baadaye. Sio wahalifuni Wakenya wanaoomba kusikilizwa. Wanastahili ulinzi, sio risasi.”

Akothee anajiunga na kikundi cha wanaharakati, wasanii na viongozi wa mashirika ya kiraia ambao wamezungumza katika wiki za hivi majuzi, wakitaka haki itendeke kwa wale ambao wamepoteza maisha au kujeruhiwa wakati wa maandamano.

Related Articles

Back to top button