Akon amtaka mkewe wamlea binti yao pamoja

LOS ANGELES: MUIMBAJI wa wimbo wa ‘Lonely’, Akona ameiomba mahakama ihakikishe kuwa yeye na mtalaka wake Tomeka Thaim wanashiriki kwa pamoja majukumu ya malezi ya binti yao.
Awali Tomeka, alifungua talaka mwezi Septemba, siku chache kabla ya kumbukumbu yao ya ndoa ya miaka 29, huku akihitaji haki ya kisheria na ya kuwa muangalizi wa binti yao wa miaka 17.
Kulingana na nyaraka za mahakama ambazo gazeti la People limezipata, wote wawili waliiomba mahakama kutompa mmoja msaada wa kifamilia wa malezi yam toto wao.

Akizungumza kwenye kipindi cha ‘The Zeze Mills’ alisema ndoa za wanawake wengi ni sehemu ya tamaduni za kiafrika.
“Kwa mimi, inaonekana kawaida, kwa kuwa ni tamaduni zetu. Hatujabadilisha tamaduni zetu za Kiafrika tunapofika nchi za Magharibi. Tatizo kubwa la dunia ya Magharibi ni kwamba walitengeneza sheria nyingi bila kuzingatia asili ya binadamu.”
Akon alisisitiza kuwa yuko pamoja na watoto wake wote na anaona kuwa ni jukumu lake kuwatunza watoto kuwa na maadili, kuelewa na kumlinda mama yao.
Aliongeza: “Jukumu langu siyo kufanya mambo ya ziada kama sherehe na maonesho ya kuimba. Ninapokuwa nikitekeleza majukumu yangu ya kuhakikisha familia yangu inapata makazi na chakula, ikiwa na nafasi ya kuonesha upendo, ndiyo, nitafanya hivyo.
Akon anaamini kuwa ndoa na uhusiano wa kimapenzi ni uhusiano halali wenye maana.
Mwanamuziki Amirror awali alidai kuwa ni miongoni mwa wake wanne wa Akon, na kuwa wote wanaishi sehemu tofauti, ikiwa ni pamoja na Atlanta, Los Angeles na Afrika.
Alisema hawawezi kuwa Pamoja kila wakati, kwa hivyo hahitaji kuwa na uhusiano wa karibu kila wakati… Akon ni mtu wa aina yake siyo wa udanganyifu. Hii ni tamaduni zetu… Kila mwanamke anataka kuwa wa pekee.”




