EPLKwingineko

Akanji mali ya Man City

Manuel Akanji akisaini mkataba

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu soka Uingereza(EPL) Manchester City imetangaza kumsajili beki wa Kiswisi Manuel Akanji kwa mkataba wa miaka mitano kwa pauni milioni 15 sawa na shilingi bilioni 40.4.

Akanji mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na City akitokea Borussia Dortmund ambako alicheza mechi 158 tangu Januari 2018.

Beki huyo amecheza michezo 41 timu ya taifa ya Uswisi na alihusika kwa kiasi kikubwa katika kufuzu kwa nchi hiyo Kombe la Dunia.

“Nina furaha kuwa hapa na siwezi kusubiri kuanza kucheza. City imekuwa moja ya timu bora barani ulaya katika misimu kadhaa iliyopita. Kwa kweli natazamia kujipima Ligi Kuu na nitafanya kila niwezalo kusaidia klabu hii kuwa na mafanikio,”amesema Akanji.

Mkurugenzi wa Soka wa Man City, Txiki Begiristain amesema: ” Manuel ana uzoefu wa kutosha wa kucheza katika kiwango cha juu cha soka la Ulaya na tuna imani ataongeza vitu vya thamani kwenye kikosi chetu.”

Related Articles

Back to top button