Ahmad Musa: Kanp Pillars tunabeba kombe la Nigeria

NIGERIA: MENEJA Mkuu mteule wa Kano Pillars na nahodha wa sasa wa Super Eagles, Ahmed Musa, amejinadi kwamba timu yake hiyo inakwenda kubeba kombe la ligi ya Nigeria kwa msimu ujao kwa kuwa washafahamu madhaifu yao na wanajua namna ya kuyadhibiti.
Akizungumza na wanahabari leo, Julai 10, siku ya Alhamisi katika uwanja wa nyumbani wa klabu hiyo mjini Kano.
Musa amesisitiza umuhimu wa uungwaji mkono na ufadhili kwa timu hiyo ili waweze kurudisha makali yaliyokuwa awali kabla timu hiyo haijayumba na kupoteza ushindani katika ligi ya Nigeria na mashindano ya kimataifa.
Aliwahakikishia wafuasi wake kwamba hatua tayari zilikuwa zikichukuliwa kuzuia kurudiwa kwa makosa ya msimu uliopita, akisema, “Tunaenda kuchukua kombe wakati huu.”
“Ninakuja na ajenda ya pointi tisa kwa klabu hii, ili kufufua matumaini ya klabu. Ndiyo maana ninawaomba wapenzi wa michezo wa Kano kutuunga mkono kikamilifu. Ninaahidi kufanya kila niwezalo kufufua klabu,” amesema Mussa.
Akikubali changamoto mbili za kutumika kama Meneja Mkuu na mchezaji anayefanya kazi, Musa alikiri jukumu hilo halikuwa rahisi. “Nitampa kila mchezaji nafasi ya kuchangia kikamilifu. Na kwa kuungwa mkono na mashabiki wetu, hatuhitaji kutegemea serikali. Pamoja nao na jezi yetu, tutapata kile kinachohitajika.”
“Kwa sasa, tunahitaji serikali kusaidia kuleta utulivu katika klabu, lakini pamoja na uongozi, tayari tumeanza kuandika barua kwa makampuni kadhaa kwa ajili ya udhamini. Hivi karibuni tutaifanya,” Musa amesema.
Akifafanua majukumu yake mawili, Musa aliongeza: “Na wacha nifafanue zaidi msimamo huu: ndani ya uwanja, mimi ni mchezaji, kocha ana haki ya kuniadhibu. Lakini nje ya uwanja, mimi ndiye bosi, kwa hivyo uwazi upo.”




