Mastaa

Afya ya Ariana Grande yazidi kuzua gumzo

MSANII Ariana Grande amezidi kuzua gumzo baada ya picha zake mpya kumuonesha kuzidi kupungua uzito kwa kasi kubwa.

Mrembo huyo ameonekana kupoteza uzito kwa miaka ya hivi karibuni, jambo ambalo limetajwa kuwa ni kutokana na kuamua kujikondesha kwa makusudi.

Aidha Madaktari wamesema kuwa picha hiyo, inayodhaniwa kuchukuliwa katikati ya Desemba akiwa na mashabiki katika onesho la filamu yake mpya ya ‘Wicked’, inaonesha kwamba upunguaji wake siyo wa kawaida bali ni dalili za matatizo ya kiafya.

Daktari Sue Decotiis, mtaalamu wa kupunguza uzito aliye na cheti cha bodi kutoka New York City, amedai kuwa kuonekana kwa mifupa yake ya mbavu na shingo ni dalili mbaya.

“Inaonekana kama amepoteza uzito mwingi kupita kiasi. Pia inaonekana kama macho yake yanatoka, jambo ambalo ni ishara ya kupoteza uzito mwingi na inaweza pia kuwa dalili ya ugonjwa wa tezi za thyroid.”

Daktari ameongeza kuwa mrembo huyo anaweza kuwa anaugua hypothyroidism, hali inayosababisha mifumo ya mwili kudorora. Dalili ni pamoja na matatizo ya kula kawaida na kupata uzito kidogo.

Related Articles

Back to top button