KwinginekoLa Liga

Barca yajiandaa na maisha bila Busquets

NYOTA wa Barcelona Sergio Busquets anatarajiwa kumaliza miaka 17 ya kucheza klabu hiyo mwisho wa msimu ujao.

Ripoti zimesema kwamba tayari timu hiyo inajiandaa na kuondoka kwa nahodha huyo wa Blaugrana.

Bodi ya Barca inatayarisha orodha ya wachezaji wanaoweza kujaza nafasi baada ya  Busquets kuondoka kabla ya kinachotarajiwa kuwa uhamisho wa mkongwe huyo kwenda Ligi Kuu ya Soka Marekani.

Wachezaji wawili wanapewa kipaumbe mbele zaidi katika orodha hiyo ambao ni Martin Zubimendi wa Real Sociedad ya Hispania na Ruben Neves wa Wolverhampton Wanderers ya Uingereza.

Zubimendi anakadiriwa kuwa na thamani ya juu na amekuzwa nyumbani lakini anaripotiwa kuwa na kipingele cha kuachiwa cha Euro milioni 60 sawa na shilingi bilioni 138.6 hali inayoweza kuleta ugumu kumsajili.

Neves anaweza pia asiwe na thamani ndogo lakini wakala wake Jorge Mendes ana uhusiano mkubwa na Barcelona jambo linaloweza kurahisisha majdiliano.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button