
TIMU ya Ihefu ya mkoani Mbeya imemteua Juma Mwambusi kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo.

Mwambusi anachukua nafasi ya Zuber Katwila.
“Tumefikia makubaliano na Kocha Juma Mwambusi kuwa Kocha wetu mkuu ndani ya timu yetu ya Ihefu Sc,”imesema taarifa ya klabu hiyo.
Ihefu imesema Mwambusi ameungana na benchi la ufundi la awali la timu hiyo katika kufanikisha malengo ya klabu kufanya vizuri katika Ligi kuu na michuano mingine.