Filamu

Anna: Serikali iwekekeze katika Sanaa

DAR ES SALAAM: Mwigizaji wa Filamu nchini Godliver Gordian ‘Anna’ amesema Serikali inapaswa kuwekeza kwenye sanaa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Anna amesema kuwa nchini Korea Serikali imewekeza kwa asilimia kubwa kwenye tasnia ya sanaa hali inayosababissha kufanya vitu vikubwa zaidi hivyo anatamani  na Tanzania iige mfano huo.

“Serikali imeangalia na ikatambua ndio sababu Rais Samia akatupeleka nchini South Korea kujifunza na tumegundua Bahari ni kubwa Samaki ni wengi kila mtu avue kwa nafasi yake katika kuleta maendeleo katika Tasnia ya Filamu.

“Wasanii tukiwa pamoja na kushirikiana tukaishi kwa Umoja tutasaidia tasnia iende mbele na kufanya kazi kwa bidii.”amesema Anna

Related Articles

Back to top button