Steve Mweusi: Joti alinivutia kwenye sanaa

MCHEKESHAJI maarufu nchini Steve Moses ‘Steve Mweusi’ amemtaja mchekeshaji Lucas Mhuvile maarufu kama Joti kuwa ndiye aliyemvutia kuingia kwenye sanaa hiyo.
Akizungumza na HabariLEO mapema leo Steve amesema alivutiwa na Joti kutokana na ubunifu wake alionao kwa muda mrefu kwenye uchekeshaji hata hivyo amefanikiwa kudumu kwenye sanaa hiyo kwa muda mrefu.
“Joti amenisaidia pia kimawazo ni mtu ambaye ukikwama anakusaidia hana shida tuliwahi kujadili wazo moja akanipa ushauri mzuri tu, kwahiyo ni mtu ambaye hana tabu kabisa,” amesema Steve.
Amesema cha kipindi cha ‘Ze Comedy Show’ mwaka miaka ya 16 iliyopita ndipo alipoaanza kumuona Joti na kutamani sanaa ya uchekeshaji.
“Halafu kingine Joti amedumu sana kwenye tasnia, halafu kwenye ubora ule ule ni mtu safi kwenye ujuzi sana kwenye kazi,” ameongeza.