Ligi Daraja La Kwanza
Nyigu: Ninapenda kucheza kuliko kuimba

DAR ES SALAAM: Dansa katika video za wasanii wa Bongo fleva Angel Nyigu amesema kuwa anapenda sana kucheza hivyo hawezi kuingia kwenye kuimba nyimbo kama wanavyofanya wengine.
Angel amesema kuwa mshika mawili moja umponyoka kwa upande wake anapenda zaidi kipaji chake cha kucheza kuliko kuimba.
“Kucheza ndio sanaa iliyonitambulisha na kunifanya kwenda nchi mbalimbali kutokana na kucheza kwangu, sina mpango wa kuingia kwenye kuimba nitacheza tu na ndicho ninachopenda zaidi ya vyote.”amesema msanii huyo.




