Kwingineko
Real vs Atlético nusu fainali Super Cup

Real Madrid na Atlético Madrid zitakiwasha leo katika nusu fainali ya kwanza ya Super Cup 2024 ya Hispania mechi itakayopigwa Saudi Arabia.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Al-Awwal Park uliopo jiji la Riyadh.
Nusu fainali ya pili itakuwa kati ya Barcelona na Osasuna Januari 11.
Washindi wa nusu fainali hizo watakutana fainali itakayofanyika Januari 14
Kwingineko Liverpool leo itakuwa mwenyeji wa Fulham katika nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Carabao huko England.
Katika michezo ya kirafiki ya kimataifa leo ni kama ifuatavyo:
DR Congo vs Burkina Faso
Afrika Kusini vs Lesotho
Saudi Arabia vs Hong Kong
Tunisia vs Cape Verde